Tatizo la kuwahi kufika kileleni husumbua wanaume wengi.
Kwa kuwa tatizo hili linafahamika vizuri kwa sasa, ni muhimu tukiwekeza nguvu na maarifa katika kutafuta jawabu lake. Tumejaribu kutafuta suluhu yake.
Baadhi ya njia zinazoweza kutumika kwenye kukabiliana na changamoto ya kuwahi kufika kileleni ni hizi;
1. Virutubisho
Virutubisho vya zinc, foliki asidi na magnesium husaidia kutatua changamoto hii.
Huongeza uzalishwaji wa vichocheo vya kiume kwa mhusika yaani testosterone ambayo inaweza kutibu changamoto ya kuwahi kufika kileleni hasa ikiwa inasababishwa na upungufu wa nguvu za kiume. (1,2)
Virutubisho hivi huuzwa madukani pasipo kuhitaji cheti cha daktari.
Unaweza kuamua kuvinunua ili vikusaidie.
2. Maandalizi
Utafiti mmoja uliohusisha wanawake 1,055 wenye umri wa kati ya miaka 18-94 unaonesha kuwa asilimia 18 pekee ya wanawake wote ndiyo hufika kileleni kwa kushiriki tendo la ndoa pasipo uwepo wa michezo na maandalizi ya kabla.
Asilimia 37 ya wanawake hufika kileleni baada ya kuandaliwa kwanza kabla ya kushiriki tendo la ndoa.
Maandalizi haya yalihusisha kuchezea sehemu ya kisimi cha uke ambacho huundwa kwa zaidi ya neva za fahamu 8000.
Hii inamaanisha kuwa kupitia michezo hii, ni rahisi kwa mwanamme kumfikisha mwanamke kileleni hata kama atataumia muda mchache.
Kwa mwanamme mwenyewe, michezo hii huongeza kujiamini pamoja na kuandaa mwili kikamilifu ili uweze kuhimili tendo la ndoa.
Hutengeneza uwiano mzuri wa vichocheo na saikolojia ya mwili hivyo kurefusha muda wa ushiriki wa tendo la ndoa.
3. Bana Uume
Unaukumbuka ule mstari unaotengenisha kichwa na sehemu nyingine ya uume?
Sehemu hiyo ni muhimu sana katika kuleta ahueni ya tatizo la kuwahi kufika kileleni.
Masters na Johnson waligundua njia hii mwishoni mwa miaka ya 1950. Kwa kiingereza huitwa squeeze technique.
Hufanywa vipi? Mwanamke au mwanamme mwenyewe hupaswa kujisisimua hadi pale anapokaribia kufikia kileleni, kisha huacha ghafla na kuukandamiza kidogo mstari unaotenganisha kichwa na sehemu nyingine ya uume kwa sekunde 30 kabla ya kuendelea tena.
Lengo lake ni kumfundisha mwanamme ishara na dalili za kufika kileleni ili wakati wa tendo la ndoa ajue kujizuia.
Baada ya kujisisimua mwenyewe kwa walau mwezi mmoja, tendo la ndoa hupaswa kufanyika kwa mtindo huohuo kwamba kila mwanamme akitaka kufika kileleni ni lazima asimame na kukandamiza kwa nguvu kidogo mstari husika.
Pamoja na kumfundisha mwanamme udhibiti, kitendo hiki pia hupoozesha usafirishwaji wa taarifa pamoja na msisisimko mkubwa wa kichwa cha kiume unaoweza kusababisha mwanamme afike kileleni mapema.
Huitwa squeeze techinque.
4. Sitisha Kwanza
Jambo kubwa la kushukuru ni kuwa mtu mwenye changamoto hii hujua kabisa kuwa yeye ni mhanga.
Uelewa huu una faida katika kumfanya awe makini katika kujidhibiti.
Kusimamisha tendo la ndoa kisha uume ukatolewa nje ya uke kwa walau sekunde 30 kabla ya kuendelea tena hupunguza ukubwa wa msisimko unaosababisha mwanamme awahi kufika kileleni.
5. Mazoezi
Mwaka 1948 mazoezi ya Kegel yalianzishwa rasmi na Dr. Arnold Kegel ili kuimarisha misuli ya sakafu ya nyonga.
Mazoezi haya hufaa sana kwenye kuboresha changamoto za mfumo wa mkojo pamoja na uzazi kwa wanawake na wanaume.
Mazoezi ya Kegel yamethibitishwa na tafiti kuwa na uwezo wa kutibu changamoto ya kuwahi kufika kileleni. (3,4)
6. Punyeto
Tumeelezea mara nyingi kuwa punyeto haina athari za moja kwa moja kwenye kupunguza nguvu za kiume pamoja na kumfanya mwanamme awe na tatizo la kuwahi kufika kileleni.
Unafahamu kwa nini kufika kileleni kwa mara ya pili huchelewa zaidi kuliko jinsi inavyotokea kwa mara ya kwanza wakati wa kushiriki tendo la ndoa?
Kwa sababu mwili huwa umezoea hali hii, na muda inaotumia kutengeneza taarifa za kubana mirija ya shahawa ili ziweze kutoka ni mrefu zaidi kuliko inavyokuwa kwa mara ya kwanza.
Upigaji wa punyeto saa 1-2 kabla ya kushiriki tendo la ndoa kumethibitishwa na tafiti kuwa na uwezo wa kuondoa changamoto ya kuwahi kufika kileleni hasa kwa wanaume wenye tatizo la uume wenye msisimko mkubwa. (5,6)
Hii haina tofauti na mtu aliyefanya tendo halisi la ndoa.
7. Ona Wanasaikolojia
Changamoto kubwa ya kuwahi kufika kileleni ni kusababisha mfadhaiko na changamoto za kisaikolojia kwa mhusika.
Saikolojia ndiyo kila kitu.
Ikiwa umepambana sana pasipo mafanikio, onana na wataalamu wa saikolojia wakupe msaada.
8. Tumia Kondomu
Kwa kutambua uwepo wa tatizo hili, baadhi ya makampuni huzalisha kondomu maalumu kwa ajili ya watu wenye changamoto hii. (7)
Kondomu hizi hutengenezwa zikiwa na uzito wa ziada tofauti na kondomu za kawaida.
Lengo huwa ni kupunguza msuguano kati ya uume na uke.
Kama huwezi kupata kondomu hizi, jaribu kutumia kondomu za kawaida. Zinaweza kukusaidia.
9. Tumia Dawa
Siyo kila mwanamme anayewahi kufika kileleni huwa na changamoto ya upungufu wa nguvu za kiume.
Sababu zingine zinaweza kuwa za kisaikolojia, stress, sonona, sababu za kimaumbile au uwepo wa baadhi ya magonjwa mfano kisukari.
Inafaa ufanye uchunguzi wa afya yako kwa kina, na ikiwa utathibitika kuwa tatizo hili linasababishwa na upungufu wa nguvu za kiume, dawa kama sildenafir zinaweza kusaidia. (8,9)
Daktari anaweza pia kushauri dawa zingine kama fluoxetine au sertraline.
Kwa wanaume ambao tatizo hili huchangiwa na kuwa na uume wenye msisimko mkubwa sana, kutumia dawa za kuupaka uume kama benzocaine, lidocaine au prilocaine husaidia kutatua tatizo hili kwa ufanisi mkubwa.
Dawa hizi ni hatari kwa afya. Zinaweza kusababisha matatizo makubwa ikiwa ni pamoja na kuongeza ukubwa wa tatizo ikiwa hazitatumiwa vizuri.
Ni muhimu kupata ushauri wa daktari au mfamasia kabla ya kuamua kuzitumia.
10. Badili Mawazo
Mwamsho wa hisia za kushiriki tendo la ndoa huanzia kwenye ubongo.
Kadri unavyotumia nguvu kubwa kufikiria kitendo hiki ndivyo kwa namna hiyo hiyo ubongo huzalisha kemikali na vichocheo vingi zaidi.
Kuwaza mambo mengine yasiyo na uhusiano na tendo la ndoa huupa ubongo kazi nyingine ya ziada katika utendaji wa kazi yake.
Ni sawa na wewe uanze kufua huku unapika, wakati huohuo unafanya usafi wa nyumba.
Muda utakaotumia kumaliza zoezi la kufua ni mrefu zaidi wakati kwenye mazingira haya ni mrefu zaidi kuliko kama ungeamua kufua kwanza kisha uendelee na mambo mengine.
11. Fanya Taratibu
Ukitaka kushinda mbio za umbali mrefu, miongoni mwa mambo ya msingi unayopaswa kufanya ni kuanza mbio hizo taratibu ili mwili ujiandae kumaliza mbio hizo kwa kasi.
Hali ipo hivyo pia kwenye tendo la ndoa. Kufanya tendo hili kwa haraka sana ni mojawapo ya sababu za kufika kileleni haraka.
Jambo hili hutengeneza msisimko mkubwa kwenye neva za fahamu za kichwa cha uume ambazo hukaridiwa kufikia 4000.
Punguza kasi yako.
12. Vyakula Mbadala
Vyakula kama tikiti maji, vitunguu saumu, asali, spinach, tangawizi na chocolate nyeusi hufanya kazi kama zilivyo viagra za madukani.
Vyakula hivi kwa ujumla wake hufahamika zaidi kama viagra za asili.
Hupatikana karibia kila sehemu na gharama ya kuvipata ni ndogo.
Viongeze kwenye lishe yako.
Muhtasari
Tatizo la kuwahi kufika kileleni linatibika.
Jaribu kufuata njia hizi ambazo kwa kiasi kikubwa zitakusaidia sana kurejesha heshima ya ndoa kwa mara nyingine.