Ni hali inayoambatana na kutoka kwa damu baada ya kuisha kwa hedhi ya kawaida, au kabla ya kuanza kwa hedhi.
Jambo hili linapotokea, mwanamke ataona damu kidogo ambayo anaweza kuitambua kwa kutazama nguo yake ya ndani, au pia inaweza kutoka damu nyingi kabisa mithili ya hedhi.
Sababu
Huwa kuna sababu nyingi zinazoweza kuwa chanzo cha kutokea kwa tatizo hili.
Miongoni mwa sababu hizo ni matumizi ya njia za kisasa za uzazi wa mpango mfano kitanzi, majira, vijiti na sindano za depo provera, matumizi ya baadhi ya dawa mfano p2, kuharibika kwa ujauzito, magojwa ya zinaa mfano kisonono, klamidia na kaswende, ajali zinazohusisha sehemu ya uke, pia tendo la ndoa hasa uke unapokuwa mkavu sana, uvimbe kwenye sehemu za mfumo wa uzazi, aina fulani za saratani, hasa ile ya mlango wa kizazi, Mvurugiko wa homoni pamoja na msongo wa mawazo.
Changamoto hii inaweza kuambatana pia na dalili za maumivu makali ya sehemu ya chini ya tumbo, kiuno na mgongo, uchovu mkubwa, kizunguzungu pamoja na homa.
Muhtasari
Onana na daktari ili akushauri, akuchunguze na ikiwezekana akupatie tiba kwa kadri atakavyoona inafaa.