Athari za Juisi za Wiwandani kwa Watoto

2 Min Read

Mwongozo wa American Academy of Pediatrics (AAP) unaelekeza kuwa mtoto asipatiwe juisi za matunda hadi afikishe walau umri wa mwaka mmoja.

Jambo hili husababisha kutokea kwa utapiamlo kwa kuwa juisi huwa hazina kiwango cha kutosha cha protini, vitamini pamoja na madini chuma, calcium na zinc.

Aidha, inaweza kusababisha udumavu, kuoza kwa meno, kuzidi kwa uzito wa mwili pamoja na kuhara.

Tahadhari

Baadhi ya juisi hasa zile za viwandani huwa na kiasi kikubwa cha viambato vya sorbitol ambavyo hujulikana pia kwa majina ya D-sorbitol, 50-70-4, E420 au D-glucitol.

Hii ni aina ya wanga ambao huwekwa kwenye kundi la sukari zenye asili ya pombe.

Watoto huwa hawawezi kuvifyonza mwilini mwao hivyo huwafanya wapatwe na matatizo ya kuhara, tumbo kujaa gesi pamoja na maumivu ya tumbo na kichwa. Watoto wasipatiwe juisi hizi.

Ushauri

Kwa kuwa baada ya kufikisha miezi 6 watoto huanza kupatiwa vyakula mbadala, baadhi ya wazazi huanza kuwapa pia juisi.

Badala ya kumpatia juisi, inashauriwa apatiwe matunda kamili pamoja na mboga za majani zilizopikwa.

Huwa na virutubisho vingi ambavyo haviwezi kupatikana kwenye juisi za matunda.

Hata hivyo, kwa kuwa watoto wengi wanapokuwa na miezi 6 huwa bado hawajaota meno, unaweza kuwapa juisi kwa kuzingatia masharti haya;

  • Iwe juisi halisi ya matunda
  • Isiwe juisi ya viwandani, au unga unaochanganywa nyumbani ili kuitengeneza
  • Isizidi kiasi cha 120 ml kwa siku
  • Mpatie anywe ikiwa kwenye kikombe, sio kwenye chupa
  • Mpe katikati ya mlo pekee

Hali ya usafi inapaswa kuzingatiwa wakati wa maandalizi ya juisi hii.

Uwepo wa aina yoyote ya uchafu unaweza kuwa chanzo cha magonjwa kwa mtoto ambaye kwa umri huu mfumo wa kinga za mwili huwa bado haujakomaa vizuri.

Hakikisha unazingatia mambo ili kudumisha afya bora kwa mwanao.

Share This Article