Omega 3: Mafuta ya Asidi yenye Faida lukuki kwa Afya

4 Min Read

Asidi za mafuta ya Omega 3 zimepata umaarufu mkubwa sana siku za hivi karibuni.

Hivi ni virutubisho vinavyopatikana kwa wingi kwenye aina mbalimbali za samaki, mbegu za chia pamoja na vyakula jamii ya karanga.

Unaweza kupata kirutubisho hiki kwa kutumia vyakula husika, lakini zaidi unaweza kutumia virutubisho vinavyopatikana kwa njia ya vidonge maalumu.

Mafuta haya huwa na faida zifuatazo kwa afya ya binadamu;

1. Saratani

Unapozungumzia magonjwa makubwa, hatari na yanayoua watu wengi duniani hauwezi kusahau kutaja saratani.

Kuna aina nyingi sana za saratani zinazompata binadamu na asidi za mafuta ya Omega 3 zimetajwa na tafiti kuwa na uwezo wa kuzikinga pamoja na kupunguza athari zake. (1,2)

Mfano ni saratani ya tezi dume, utumbo mkubwa, saratani ya damu pamoja na saratani ya matiti

2. Usingizi

Unapozungumzia changamoto kubwa zinazo ikabili dunia ya sasa, hauwezi kusahau kutaja tatizo la kukosa usingizi.

Unaweza kuboresha usingizi kwa kutumia virutubisho hivi.

Hufanya kazi kwa kuisaidia mifumo inayo ratibu usingizi, hivyo kuharakisha upatikanaji wa usingizi pamoja na kuufanya usingizi huo uwe bora, usio sumbua. (3)

3. Ngozi

Virutubisho hivi ni muhimu sana hasa kwa watoto ambao mabadiliko ya hali ya hewa huwasumbua sana.

Husaidia kutibu changamoto mbalimbali za ngozi, kufungua vinyweleo vya ngozi, kuondoa ukavu wa ngozi pamoja na kuondoa makunyanzi. (4,5)

Vinapaswa kutumika kwa watoto wenye umri zaidi ya miezi 6 na si vinginevyo.

4. Ubongo

Mwanamke anaweza kutumia kabla hata ya kupata ujauzito, na anaweza kuendelea kutumia wakati na baada ya kujifungua.

Watoto wenye umri wa miezi 6 na kuendelea wanaweza pia kupatiwa virutubisho hivi.

Husaidia ukuaji bora wa ubongo, pamoja na kuupa uwezo wa ziada katika kuchambua mambo mbalimbali. (6)

Unataka mtoto wako awe na uwezo mkubwa darasani? Pamoja na kufuata kanuni zingine za utunzaji bora wa ujauzito, hakikisha unatumia virutubisho hivi.

5. Uvimbe

Uvimbe ni tendo linalochochewa na mwamsho wa kinga za mwili na linaweza kutokea kutokana na sababu za kimazingira au zilizo ndani ya mwili.

Virutubisho hivi huhusishwa moja kwa moja na kuudhibiti mwili katika kuzalisha vichocheo vinavyosababisha kutokea, au kuongezeka kwa uvimbe mwilini.

6. Moyo

Virutubisho hivi huulinda moyo kwa kupunguza shinikizo la damu, kuharibu mafuta mabaya pamoja na kuimarisha mishipa ya damu.

Mambo haya ni muhimu sana katika kupambana na changamoto za mshituko wa moyo, shambulio la moyo pamoja na kiharusi.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), wastani wa watu milioni 19.7 hufariki kila mwaka duniani kutokana na magonjwa ya moyo.

Takwimu hizi zinatisha, ni muhimu kujilinda.

7. Pumu

Tatizo hili huathiri mapafu, na humfanya mhusika apate changamoto kubwa katika kupumua.

Tafiti kadhaa zinataja umuhimu wa virutubisho hivi katika kupambana na pumu kwa watoto na watu wazima. (21)

Pengine hauna ufahamu wa kutosha kuhusu pumu. Ni ugonjwa mbaya, unatesa. Tumia virutubisho hivi kujilinda.

8. Maumivu ya Hedhi

Hedhi ni tendo la kibaiolojia na kiasili linalompata mwanamke kila mwezi, tangu avunjapo ungo hadi muda wa ukomo wake.

Tendo hili huwa siyo rafiki kwa wanawake wengi kwa kuwa huambatana na maumivu makali ya tumbo.

Asidi ya mafuta ya omega 3 husaidia kupunguza maumivu haya.

Ushauri

Hii sio dawa, hivyo inaweza kutumika kila siku kama sehemu ya mlo wa kawaida.

Hupatikana kwa wingi kwenye maduka ya dawa na virutubisho, unaweza kwenda huko kutafuta.

Share This Article