UHALISIA: Ultrasound ni Kipimo Salama kwa Wajawazito

1 Min Read

Ultrasound hutumia mawimbi ya sauti kutengeneza picha za ndani ya mwili.

Haitumii mionzi mikali ya mwanga au nguvu kubwa kama X rays hivyo ni salama kabisa kwa mama wajawazito. (1,2)

Ujauzito wa kawaida usio na changamoto yoyote mara nyingi huhitaji ultrasound mbili tu ambazo mara nyingi hufanyika chini ya wiki 12 na nyingine ikifanyika kati ya wiki ya 18-20.

Hii sio sheria, hivyo namba ya vipimo vyake inaweza kuongezeka kwa kadri ya uhitaji wa wakati huo

Baadhi ya wanawake hasa wale wa vijijini hujifungua bila kufanya ultrasound hata moja, huku baadhi ya wanawake wakifanya hadi ultrasound 3-4 kulingana na hali tofauti zinazokuwa zinawapata kwa wakati huo.

Jambo la msingi zaidi kujua ni kuwa ultrasound ni salama kabisa na haupaswi kuiogopa unaposhauriwa na daktari wako. (3)

Haitumii mionzi mikali, hutumia mawimbi ya sauti kutengeneza picha.

Share This Article