Sildenafil Citrate ndiyo jina rasmi la dawa hii yenye majina mengi ya kibiashara.
Baadhi ya makampuni huizalisha ikiwa na majina ya kibiashara yanayofahamika kama Viagra, Erecto, Aronix, Liberize, Nipatra, Revatio, Granpidam n.k
Matumizi
Dawa hii iligundiliwa mwaka 1989 wakati kampuni ya Pfizer ikifanya utafiti wa kutengeneza dawa ya kutibu shinikizo la juu la damu pamoja na maumivu ya kifua yanayo sababishwa na ugonjwa wa moyo. (1)
Pamoja na kazi hizi, Sildenafil Citrate hutumika pia katika kutibu tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.
Madhara
Viagra inaweza kuleta maudhi ya kusababisha maumivu makali ya kichwa, kubadilika kwa mapigo ya moyo, kiungulia, kuishiwa kwa pumzi, kupungua kwa uoni wa macho, kupungua kwa uwezo wa kusikia pamoja na kuvujia puani kwa damu. (2,3)
Aidha, dawa hii inaweza kuua kwa kushusha shinikizo la damu. Hii inaweza kutokea hasa pale inapotumika pamoja na dawa zinazopatikana kwenye kundi la nitrates. (4)
Katika visa vichache, viagra huhusishwa na kuvujia kwa damu kwenye ubongo wa baadhi ya wanaume hivyo kusabisha kifo. (5)
Muhtasari
Umakini mkubwa unahitajika wakati wa matumizi ya dawa hii.
Ni muhimu kupata ushauri wa daktari au mfamasia kabla ya kuamua kuitumia.