Ugonjwa wa ajabu unaripotiwa kuingia nchini Tanzania.
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mh Samia Suluhu Hassan, akizungumza kwenye mkutano wa Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Katoliki Afrika Mashariki na Kati – AMECEA amesema kuwa serikali inafanya uchunguzi wa kuzuka kwa ugonjwa wa ajabu kwenye mikoa ya kusini unaofanya watu watokwe na damu puani pamoja na kudondoka.
“Angekuwa mmoja wawili tungesema presha imepanda, veins zime burst anatokwa na damu za pua. Lakini ni wengi. Ni maradhi ambayo hatujawahi kuyaona” – Rais
Kutokana na uwepo wa hali hii, uchunguzi wa kina unaendelea ili kujua undani wa changamoto hii mpya.
Hata hivyo, Rais amesisitiza Watanzania wote kutunza mazingira kwani baadhi ya magonjwa haya hutokana na uharibifu wa mazingira asilia.
Tanzania ni mwenyeji wa mkutano mkuutano wa 20 wa AMECEA unaoongozwa na kauli mbiu “Utunzaji wa Mazingira kwa Ajili ya Maendeleo Endelevu ya Binadamu.”
Hii ni kauli mbiu inayochota maudhui yake kutoka katika Waraka wa Kitume wa Kiongozi mkuu wa kanisa hilo Baba Mtakatifu Francisko, “Laudato si” yaani “Sifa iwe kwako” juu ya utunzaji wa nyumba ya wote.”