Virusi vya Ugonjwa wa Mpox Vyagunduliwa Kwenye Shahawa

2 Min Read

Masalia ya vinasaba vya ugonjwa wa homa ya nyani yamegunduliwa kuwemo kwenye baadhi ya shahawa za wanaume waliothibitika kuwa na ugonjwa huo.

Ripoti hii inazua wasiwasi mpya juu ya uwepo wa uwezekano wa ugonjwa wa homa ya nyani kuwa unasambazwa kupitia tendo la ndoa.

Hadi sasa, WHO pamoja na CDC haziitambui kuwa hii ni mojawapo ya njia zinazosambaza ugonjwa husika.

Kwa mujibu wa takwimu za Juni 14, ugonjwa huu umesambaa kwenye nchi 39 duniani, 32 kati yake ikiwa ni mpya kabisa ambazo hazijawahi kuwa na visa vyake kabla.

Aidha, zaidi ya watu 1600 wamethibitika kuambukizwa na visa vingine vipya 1500 vikiendelea kuchunguzwa. Ili kuhakikisha kuwa dunia inachukua hatua stahiki katika kupambana na ugonjwa huu, Juni 23 WHO itakaa kujadili ikiwa iutaje ugonjwa huu kuwa janga la dharura linalohitaji uangalizi wa kimataifa au la.

Hatua hii inakuja baada ya kutokea usambaaji wa kasi usio wa kawaida hasa kwenye maeneo mapya ambayo kihistoria hayajawahi kuwa na visa vya ugonjwa huu.

Historia

Mwaka 1958, nyani wawili waliokuwa wanafugwa kwa ajili ya shughuli za kitafiti walipatwa na tatizo la kutokwa na vipele vikubwa mwilini.

Aina hii ya vipele inafanana na ile ya ugonjwa wa ndui na tetekuwanga.

Hii ndiyo sababu iliyofanya ugonjwa huu ukaitwa ugonjwa wa virusi vya nyani, au monkeypox disease.

Hadi leo Juni 1, 2022, watu 72 duniani wamethibika kupoteza maisha tangu mlipuko wa mwezi mei uripotiwe.

Share This Article