UHALISIA: Asali si Salama kwa Watoto Chini ya Umri wa Mwaka Mmoja

2 Min Read

Asali ni chakula chenye manufaa makubwa sana kwa afya ya binadamu.

Viambato vikubwa viwili vya asali ni maji na sukari.

Kwa mujibu wa Idara ya Kilimo ya Marekani (USDA), asali huwa na nishati ya kutosha, protini, wanga, madini ya chuma, calcium, magnesium, phosphorus, zinc, copper, fluoride na selenium.

Hivyo ni baadhi ya virutubisho vichache tu kati ya vingi.

Uhalisia

Pengine katika pitapita zako utakuwa umewahi kusikia kuwa chakula hiki si salama kwa watoto. Uliamini madai haya

Ni kweli kuwa asali haifai kutolewa kwa watoto wenye umri chini ya mwaka mmoja kwa kuwa mfumo wao wa kinga, pamoja na ule wa chakula huwa haujakomaa vizuri.

Chakula hiki huwa na asilimia kubwa ya kubeba bakteria wabaya jamii ya Clostridium botulinum ambao kwa umri huo, mtoto huwa hawezi kuwaharibu akiwala.

Husababisha tatizo hatari lisilo onekana mara kwa mara linaloitwa Infant botulism ambalo huwa na dalili za choo kigumu, kuweweseka, kifafa, changamoto za kupumua zinazosababishwa na kupooza kwa mfumo wa hewa na hatimaye kifo ikiwa msaada wa haraka hautatolewa (1,2,3)

Epuka kuwapatia asali watoto wenye umri huo ili kuwalinda.

Muhtasari

Watoto wenye zadi ya mwaka mmoja, watu wazima, wanawake wajawazito pamoja na wazee wanaweza kutumia asali kwani miili yao huwa imekomaa vya kutosha kupambana na bakteria hawa.

Iwe ni nyuki wadogo au wakubwa, nunua asali utumie.

Share This Article