UHALISIA: Tohara Haipunguzi Ukubwa wa Uume

2 Min Read

Tofauti na jinsi ambavyo watu wengi huamini, tohara haiwezi kudumaza afya ya sehemu za siri za mwanamme hasa ainapofanywa kwa mtoto mchanga.

Ukuaji wa viungo vyote vinavyounda mwili wa binadamu huongozwa na mifumo rasmi iliyoshikizwa kwenye vinasaba vya urithi pamoja pamoja homoni mbalimbali.

Msingi wa taarifa hizi hauwezi kuathiriwa kwa kukata ngozi ya mbele inayofunika sehemu hizo.

Ni Asili

Kama ambavyo mtu huzaliwa akiwa na asili ya urefu, ufupi, macho makubwa au kipara na asiwe na uwezo wa kuibadili asili hii, vivyo hivyo kwa ukubwa au udogo wa maungo haya muhimu kabisa kwa afya ya uzazi wa mwanamme. (1,2)

Tohara haiwezi kwa namna yoyote ile kuathiri ukuaji wa sehemu za siri za mwanamme pamoja na kupunguza msisimko wa tendo la ndoa kwa sababu kinacho ondolewa ni ngozi tu, siyo kichwa wala nyama ya sehemu hizo. (3)

Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali, miongozo ya Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) pamoja na kituo cha Udhibiti na Kinga ya Magonjwa (CDC), tohara huwa na faida nyingi kwa afya ya mwanamme mwenyewe, pamoja na mwanamke ambaye atashiriki naye tendo la ndoa.

Tohara hupunguza nafasi ya kupata maambukizi ya mara kwa mara kwenye mfumo wa mkojo hasa kwa watoto wadogo. (4)

Hata hivyo, ni muhimu kukumbuka kuwa tohara siyo kinga ya magonjwa ya zinaa.

Saratani ya uume ni tatizo lisiloonekana sana, lakini hutokea kwa baadhi ya wanaume.

Tohara husaidia kutoa kinga dhidi ya tatizo hili.

Muhtasari

Unaweza kuongeza au kupunguza urefu wa vidole vyako kwa kukata kucha?

Bila shaka hauwezi.

Huu ni mfano usio halisi sana, lakini una maana kuwa katika kuonesha kuwa ngozi inayofunika uume ni sawa tu na kucha za vidole ambavyo vikiondolewa havina athari yoyote kwenye ukuaji wa viungo husika.

Share This Article