Kama ilivyo kwa tampon, kikombe cha hedhi huingizwa pia ukeni.
Badala ya kuifyonza, kikombe cha hedhi huichukua damu hii na kuihifadhi ndani yake kabla haijatoka nje ya tundu la uke.
Muundo
Hutengenezwa kwa viambato laini vya mpira au silicone.
Huja na seti nzima itakayotumika kwenye kukisafisha na kukitakasa baada ya matumizi yake.
Usalama
Mara nyingi huwa hakina madhara kwa mtumiaji, isipokuwa kwa wale wenye mzio na silicone au mpira.
Ikiwa una hali yoyote inayooufanya uwe na mzio na mpira au silicone haushauriwi kutumia vikombe vya hedhi.
Ushauri
Changamoto yake huwa ni wakati wa kukitoa nje ambao huhitaji utulivu miubwa ili damu isimwagike.
Ni vizuri ukifanya huku umekaa kwenye tundu la choo ili iwe rahisi kumwaga damu pamoja na kukisafisha.
Muda sahihi wa kubadilisha kikombe hiki ni saa 10-12.