Pedi: Aina, Usalama na Ushauri

2 Min Read

Hufahamika zaidi kama pads au taulo za kike.

Ni bidhaa iliyotengenezwa na uwezo wa kufyonza damu ya hedhi na huvaliwa pamoja na nguo ya ndani.

Aina

Hutengenezwa kwa jinsi tofauti, zikiwa na harufu au bila harufu, kubwa au ndogo, zinazotumika mara moja au zaidi ya mara moja.

Ikiwa mtumiaji ataamua kununua zinazotumika mara moja, ataswa kuiteketeza baada ya matumizi.

Kwa wale wanaonunua pedi zinazotumika zaidi ya mara moja huwa na utaratibu wa kuzifua kabla ya kuzitumia kwa mara nyingine.

Muda unaoshauriwa kubadili taulo hizi ni kila baada ya masaa 4 hadi 8.

Muda wa Matumizi

Mhusika anapaswa kuchangua aina ya taulo ya kike inayokidhi haja yake kulingana na wingi wa damu anayotoa, uwezo wa taulo husika katika kufyonza damu pamoja na ukubwa wake.

Usalama

Utaratibu unaoongoza utengenezaji wa biadhaa hizi huhakikisha kuwa bidhaa husika zinatengenezwa kwa ubora na usalama mkubwa.

Baadhi ya taulo hizi huwa na harufu au hufungwa na deodorant ndani yake ili kukata harufu.

Wanawake wanaochagua kutumia aina hii ya pedi wanapaswa kuwa makini kwa kuwa nyingi husabaisha miwasho ukeni, na baadhi huwasababishia kutokea kwa vipele.

Ushauri

Ni muhimu kubadili pedi mapema ili kutunza usafi, pamoja na kuepusha maambukizi ya damu yanayoweza kutokea kutokana na kuzaliana kwa bakteria waliopo kwenye damu.

Aidha, wanawake wanaotumia pedi za kufua wahakikishe wanazifua vizuri pamoja na kutunza usafi wa hali ya juu ili kuepusha maambukizi.

Share This Article