Metronidazole hufahamika zaidi kama flagyl.
Ni dawa inayotumika kutibu aina mbalimbali za magonjwa yanayosababishwa na bakteria pamoja na vimelea vingine.
Pombe
Unapokuwa unatumia metronidazole hauruhusiwi kabisa kunywa pombe.
Matokeo ya muunganiko wake kwa baadhi ya watu huwa siyo mazuri.
Hutengeneza muingiliano ambao kitaalamu hufahamika kama disulfiram like reaction.
Inaweza kusababisha kiungulia kikali, kutapika, kuongezeka kwa mapigo ya moyo, maumivu makali ya kichwa, kushusha presha, degedege pamoja na kifo. (1,2)
Unaweza kutumia pombe baada ya saa 48.
Muhtasari
Metronidazole ni dawa iliyo na ufanisi mkubwa katika kutibu magonjwa mengi. (3)
Imeanza kutumika tangu mwishoni mwa miaka ya 1950.
Unashauriwa kufuata ushauri na taratibu sahihi za matumizi ya dawa hii ili kuepuka athari mbaya zinazoweza kutokea kwa afya yako.