Dawa za Asili na Kisasa za Kuondoa Chunusi na Makovu

8 Min Read

Chunusi ni tatizo la kawaida la ngozi linalotokana na kuziba kwa matundu ya ngozi kunako sababishwa na vivyweleo, mafuta, bakteria au pia mabaki ya ngozi mfu.

Kuziba huku hufanya ngozi ya eneo husika ivimbe kwa ukubwa na rangi tofauti. 

Ni tatizo la kawaida la ngozi linalokabili walau asilimia 80 ya watu wenye umri kati ya miaka 11-30 na asilimia 9.4 ya watu wote duniani.

Chunusi nyingi hupona zenyewe tu au baada ya kutumia aina fulani ya tiba pasipo kuacha makovu. Lakini, baadhi yake hugeuka kuwa sugu, hukawia kupona na huacha makovu kwenye sehemu husika.

Baada ya kutafuta suluhisho la kuondoa shida hii kwa muda mrefu pasipo mafanikio, leo tumekuletea habari njema.

Inahusu nini? Njia unazoweza kutumia kuondoa tatizo hili.

Twende pamoja.

1. Chai ya Rangi

Majani ya chai ya rangi husaidia katika kutibu chunusi, pamoja na kuondoa makovu ya chunusi.

Tafiti kadhaa huhusisha uwezo nguvu ya kuondoa chunusi na uwepo wa kemikali za polyphenols. (1,2,3)

  • Chemsha majani yake kwa dakika 5
  • Poza maji hayo
  • Tumia maji ya chai kunawa uso, kisha paka majani yake usoni
  • Acha majani hayo kwa nusu saa kisha jisafishe uso
  • Unaweza pia kutumia asali ili utengeneze scrub ya majani ya chai
  • Paka mara mbili kwa siku

2. Mdalasini

Ili mdalasini ukuondolee chunusi inabidi unga wake uchanganywe na asali. Kama ilivyo kwa mdalasini, asali pia huwa na tabia ya kupambana na bakteria.

Kutumia viambata hivi kwa wakati mmoja kutakupa faida kubwa zaidi, bakteria wote wanaosababisha kutokea kwa chunusi wataondolewa. (4,5,6)

  • Changanya vijiko viwili vya asali na kijiko kimoja cha unga wa mdalasini
  • Paka mchanganyiko huu usoni, uache kwa nusu saa
  • Jisafishe uso
  • Fanya mara mbili kwa siku

3. Aloe Vera

Utakubaliana na mimi kuwa bidhaa nyingi za urembo siku hizi hutengenezwa kwa kutumia mmea huu.

Huwa na kemikali za sulfur na salicylic acid ambazo kwa miongo mingi sasa zimekuwa zinatumiwa na wanasayansi kwenye kutibu chunusi.

Changamoto kubwa ni ladha yake, pamoja na kutengeneza gundi kali usoni. Unapaswa kuwa mwangalifu. (7,8,9)

  • Kata shina la mti wake, chukua nta yake
  • Paka usoni, usiiache ikauke sana
  • Jisafishe baada ya dakika 15 kwa maji safi
  • Fanya hivi mara mbili kwa siku

4. Apple Cider Vinegar

Uwepo wa asidi asilia za citric na lactic ndiyo nguvu sababu kuwa inayofanya apple cider vinegar itumike kutibu chunusi.

Kama haujawahi kuiona, nenda supermarket au duka lolote kubwa uulizie, utaipata.

Huwa na uwezo wa kuua bakteria wanaosababisha chunusi, pamoja na kuondoa makovu yake. (10)

  • Changanya kijiko kimoja cha apple cider vinegar pamoja na vijiko vitatu vya maji
  • Paka usoni kwa kutumia kitambaa au pamba safi
  • Iache kwa dakika moja kisha jisafishe. Usizidishe muda huo, inaweza kuunguza ngozi
  • Fanya hivi mara mbili kwa siku

5. Mafuta ya Samaki

Kwa maoni yangu, mafuta ya samaki ni miongoni mwa bidhaa za virutubisho zinazo uzwa sana kwa sasa, pia zimepata umaarufu mkubwa miaka ya hivi karibuni.

Mafuta haya huwa na utajiri mkubwa wa makundi mawili ya asidi ya Omega 3 ambayo ni eicosapentaenoic acid (EPA) na docosahexaenoic acid (DHA). 

Kemikali hizi hupambana na uvimbe, hutibu changamoto mbalimbali za ngozi kama mzio, pumu pamoja na kupambana na chunusi. (11,12)

Zipate leo madukani, au tumia kwa wingi samaki wa baharini.

6. Stress

Najua umeshangaa sana. Stress inaingiaje hapa? 

Ni kweli wala siyo uongo. Stress husababisha chunusi, pamoja na kuongeza ukubwa wa tatizo kwa wale ambao tayari wanazo.

Ni ngumu kuishi maisha yasiyo na tress lakini jitahidi walau uzipunguze.

7. Mafuta ya Nazi

Kama unataka kufahamu ni wapi unaweza kupata kemikali za lauric acid kwa wingi basi leo nakupatia jibu. Ni kwenye mafuta ya nazi.

Tafiti nyingi zinafafanua uwezo wa kemikali hii katika kupambana, kuua na kudhibiti bakteria wanaosababisha tatizo la chunusi.

Aidha, huwa na uwezo wa kuponya makovu yaliyotokana na uponaji mbovu wa chunusi. (13,14)

Mafuta asili ya nasi ambayo hayajapikwa ndiyo hufaa zaidi kwa kazi hii. 

8. Manjano

Wengi hutumia manjano kwenye kupikia, kama sehemu ya kiungo cha chakula.

Mzizi huu hutumika kutibu changamoto nyingi sana za ngozi, chunusi na makovu vikiwemo. (15,16)

  • Changanya kijiko kimoja cha manjano pamoja na vijiko viwili vya maji, asali au mafuta ya nazi
  • Paka usoni kisha acha kwa nusu saa
  • Jisafishe kwa maji masafi
  • Fanya hivi mara mbili kwa siku

9. Ndimu au Limao

Unaweza kutumia ndimu au limao kuondoa tatizo hili. Unadhani kwa nini?

Matunda haya pamoja na sifa zingine huwa na uwezo wa kuondoa sumu pamoja na kupambana na vimelea vya magonjwa.

Tafiti kadhaa huhusisha sifa hizi na matumizi yake katika kuponya chunusi. Uwepo wa vitamini E ambacho ni kiondoa sumu, na vitamini C ambayo ni nzuri kwa kinga ya mwili ndiyo silaha kuu. (17)

  • Kausha maganda yake kisha yasage yawe unga
  • Changanya unga huu na asali, maji au mafuta ya nazi kutengeneza scrub
  • Paka usoni, acha kwa nusu saa
  • Osha uso
  • Fanya hivi mara mbili kwa siku
  • Kwa ambao hawawezi kupata unga wake wanaweza kutumia ganda kujisugua, au maji yake kupaka usoni

10. Dawa

Kabla ya kuamua kutumia dawa unapaswa kuonana na daktari kwanza ili akuchunguze na kukushauri.

Matumizi mabaya ya baadhi ya dawa za kuondoa chunusi husababisha usugu wa vimelea vya magonjwa, pamoja na kuharibu ujauzito, au kufanya mwanamke apate ujauzito wa mtoto mwenye ulemavu wa kudumu.

Dawa za kawaida za dirishani hasa zile zinazojumuisha kundi la viua vijasumu, dawa za kisasa za uzazi wa mpango, baadhi ya creams haza zenye jamii ya retinoids, benzoyl peroxide na azelaic acid ni baadhi tu ya mifano.

Dawa kama isotretnoin ni hatari sana. Zinapaswa kutumika kwa tahadhari kubwa hasa kwa wanawake wenye ujauzito, na wale wanaopanga kupata ujauzito. (18,19)

Kama tulivyoanza kwa kutoa tahadhari, usitumie aina yoyote ya dawa hasa zile za hospitalini pasipo kupata ushauri wa daktari au mfamasia. Ni hatari.

11. Zinc

Tafiti zinabainisha kuwa utumiaji wa madini ya zinc, iwe kwa kumeza au kupaka kwenye ngozi hupunguza uvimbe joto pamoja na kuthibiti ukuaji wa bakteria wanaosababisha tatizo hili. (20)

Aidha, uchunguzi unaonesha kuwa watu wengi wanaosumbuliwa na tatizo la chunusi huwa na kiwango kidogo cha zinc mwilini hivyo matumizi ya madini haya yanaweza kusaidia kwenye tiba.

Muhtasari

Mtu mmoja anaweza kupoza maumivu ya kichwa kwa panadol, lakini hali ikawa tofauti kwa mwingine.

Vivyo hivyo kwa njia hizi, siyo kila mtu zitamfaa. Unapaswa kujaribu njia moja baada ya nyingine. Natumaini tatizo lako la chunusi sasa linakwenda kuisha.

Aidha, nakushauri uache kuwa unapasua chunusi zako.

Kitendo hiki husababisha kutokea kwa makovu pamoja na kuongeza ukubwa wa tatizo kwa kuwa huwasambaza bakteria wabaya ambao huhusika moja kwa moja kwenye kusababisha changamoto hii.

Share This Article