Isotretinoin ni dawa ambayo pamoja na kazi zingine, hutumika kutibu changamoto ya chunusi sugu.
Iliidhinishwa kuanza kutumika kwa mara ya kwanza duniani mwaka 1982.
Madhara kwa Wajawazito
Dawa hii ni hatari kutumiwa na wanawake wajawazito, au wale wanaopanga kupata ujauzito kwa kuwa huwa na sifa ya kuharibu ujauzito, kujifungua mtoto njiti, kufariki kwa mtoto siku chache kabla ya kuzaliwa pamoja na kujifungua watoto wenye matatizo makubwa katika utengenezwaji wa viungo vya mwili.
Changamoto hizi za kuzaliwa hudumu kwa kipindi cha maisha yote ya mtoto huyu, kuanzia utoto hadi utu uzima.
Hupatikana kwa mfumo wa vidonge au cream ikiwa inatumia majina ya kibiashara (brand names) zaidi ya 100 yakiwemo A- Ret, Acneone, Acnestar, Acnon Gel, Absorica, Accutane, Amnesteem, Claravis, Myorisan, Sotret na Zenatane.
Muhtasari
Ni muhimu kuwa makini na kuepuka kutumia dawa zinazotangazwa na watu mitandaoni pasipo kujua faida na hasara zake.
Pia, pata ushauri wa mfamasia au daktari kabla ya kutumia dawa yoyote.