Mtama unaweza kuwa chakula muhimu katika kupambana na changamoto ya udumavu, pamoja na unyafuzi wa watoto.
Virutubisho
Ni chakula kinachosifika kwa kuwa na kiwango kidogo cha sukari, wingi wa vitamini A na aina mbalimbali za vitamini B, carotene, foliki asidi pamoja na madini chuma, potassium, calcium na phosphorus.
Pamoja na virutubisho hivi, mtama huwa na protini, pia niacin ambayo huwezesha utendaji kazi wa zaidi ya vimeng’enya 400 mwilini.
Faida Zake
Utafiti uliofanywa kwa watoto 1500 kwa miezi mitatu unaonesha kuwa kuwapatia watoto mtama kama mbadala wa wali na ugali huongeza kasi ya ukuaji kwa asilimia 50 pamoja na kuboresha afya zao kwa kupunguza udumavu. (1)
Mtama huwakinga pia na changamoto ya kupata ugonjwa wa kisukari pamoja na matatizo ya upungufu wa damu na viribatumbo.
Changamoto
Pamoja na uwepo wa faida nyingi za mtama, bado jamii yetu haina uelewa wa kutosha kuhusu chakula hiki.
Sio kwa watu wa kawaida pekee, bali hata kwa wahudumu wa afya. Hii ni kwa mujibu wa utafiti mmoja uliofanyika Tanzania.
Ni chakula muhimu kinachoweza kutumika katika kupambana na unyafuzi pamoja na udumavu wa watoto.