Vyanzo, Faida na Dalili za Upungufu wa Vitamini B12

2 Min Read

Hii ni vitamini inayochanganyikana na maji.

Kwa kuwa vitamini B12 huwa na madini ya cobalt ndani yake, hupewa jina la jumla linaloitwa cobalamins.

Mahitaji

Mtu mzima huhitaji kiasi cha 2.4 mcg za vitamini B12 kila siku.

Vitamini hii hupatikana kutoka vyanzo mbalimbali kama vile samaki, uyoga, nyama, maziwa, mayai pamoja na bidhaa zingine zote zilizotengenezwa kwa maziwa.

Vitamini B12 huwa haipatikani kiasili kwenye mboga za majani isipokuwa kwenye viini vya nafaka.

Faida

Mifumo mingi ya mwili huhitaji uwepo wa vitamini B12.

Husaidia utengenezwaji wa vinasaba vya binadamu (DNA), mishipa ya fahamu pamoja na chembe nyekundu za damu.

Kwa afya ya uzazi wa mwanamme, husaidia kuongeza namba, ubora pamoja na kasi ya mbegu za kiume.

Husaidia kuzuia kuharibika kwa vinasaba (DNA) vya mbegu za kiume pamoja na kuboresha afya ya macho na kuzuia upofu.

Hukinga wanawake wajawazito ili wasijifungue watoto wenye changamoto katika utengenezwaji wa viungo vya mwili, mfano mgongo wazi.

Huimarisha afya ya mifupa, huusaidia mwili kuzuia kutokea kwa tatizo la sonona pamoja na kulinda moyo.

Husaidia utengenezwaji wa ubongo na mishipa ya fahamu.

    Upungufu

    Uchache wa vitamini hii husababisha kutokea kwa upungufu wa damu mwilini.

    Husababisha pia mwili utengeneze chembe nyekundu za damu zenye maumbo makubwa kuliko kipimo cha kawaida ambazo mara nyingi huwa hazijakomaa na huwa na vinasaba dhaifu.

    Changamoto hii huitwa Megaloblastic anemia ambayo pia huhusishwa na upungufu wa foliki asidi.

    Dalili zingine za upungufu wa vitamini hii ni uchovu, kupauka kwa rangi ya ngozi, huzuni, maumivu ya kichwa, kuvimba ulimi, kupungua kwa uzito na hamu ya kula, kuhara pamoja na kuchomachoma kwa miguu na mikono

    Muhtasari

    Japokuwa vitamini hii hutunzaa na ini kwa wastani wa hadi miakan5, jitahidi utumie kila siku kwa kuwa hupatikana kwa urahisi kwenye vyakula.

    Unaweza pia kuipata kutoka vyanzo vingine, hasa kupitia virutubisho maalumu vinavyouzwa madukani vikiwa na nyongeza yake.

    Pia, watu wasiotumia bidhaa za wanyama huwa kwenye hatari kubwa ya kupatwa na upungufu wa vitamini hii. Ni muhimu kutafuta mbadala wake ili kulinda afya.

    TAGGED:
    Share This Article