Tikitimaji Hufanya Kazi kama Viagra

1 Min Read

Tikitimaji linapokuwa limeiva huwa na utajiri wa kemikali inayoitwa glutathione.

Kemikali hii huongeza mara dufu kinga ya mwili hivyo kuongeza uimara wa mfumo wa mwili katika kupambana na magonjwa.

Ili upate glutathione kwa wingi, inatakiwa utumie sehemu nyekundu ya tunda hili inayokaribiana na ganda lake la nje. Hapo ndipo hupatikana kwa wingi.

Pia huwa na amino acid zinazojulikana kama citrulline ambazo hupanua mishipa ya damu hasa ile inayopatikana kwenye via vya uzazi wa mwanamme. (1,2)

Virutubisho Vingine

Ukiondoa kemikali hizo, tunda hili huwa pia na protini, nyuzilishe, sukari, madini chuma, calcium, magnesium, potassium, zinc, copper, asidi ya foliki, vitamini A, vitamini B12 pamoja na viondoa sumu.

Hii ni kwa mujibu wa idara ya kilimo ya Marekani, USDA.

Hufanya kazi kama zilivyo viagra hivyo huitwa viagra asili.

Tunda hili linaweza kusaidia kuboresha afya ya uzazi kwa wanaume walio na matatizo katika kushiriki tendo la ndoa.

Share This Article