Tofauti na jinsi inavyoamika kwa watu wengi, maziwa hayana faida yoyote katika kutuliza maumivu au hata kutibu vidonda vya tumbo.
Maziwa hutengeneza utando kwenye sehemu za tumbo zilizo jeruhiwa hivyo kufanya maumivu haya ya tumbo yapungue kwa muda mchache.
Pia, huwa na tabia ya kusisimua uzalishwaji wa asidi za tumboni ambazo baada ya kuisha kwa utando uliotengenezwa na maziwa husababisha maumivu makali zaidi kwa wagonjwa.
Hii ndiyo sababu inayofanya wagonjwa wa vidonda vya tumbo wapitie kipindi cha maumivu makali sana ya tumbo, hasa saa chache baada ya kunywa maziwa.
Kwa kuwa maziwa ni mojawapo ya vyanzo vya virutubisho bora kabisa kwa binadamu, na baadhi ya watu hawawezi kabisa kuacha kutumia hivyo basi ni vyema yakatumika baada ya kupata mlo mwingine.
Kumbuka kuwa hata wakati huu pia yasitumike mengi sana, pia hakikisha hautumii wakati una njaa kali kwani faida ni chache kuliko ukubwa wa maumivu utakayopata.