Tuiite morning glory.
Inaweza kufanyika muda wowote, asubuhi, mchana au hata usiku.
Tendo hili halifungwi na sheria ya muda, bali huongozwa na matakwa ya mwamko wa hisia unaokuwepo wakati husika.
Pamoja na ukweli huu, tendo la ndoa huwa na faida nyingi zaidi likifanyia mapema asubuhi kabla ya kuanza kwa majukumu ya siku mpya.
Huchangamsha mwili na akili, hivyo kumfanya mhusika aamke na ari ya kutosha katika kukabiliana na changamoto zote zilizo ndani ya kazi au majukumu yanayompa ridhiki yake ya kila siku.
Baadhi ya faida zake ni hizi;
1. Wasiwasi
Hupunguza wasiwasi.
Wakati wa kufika kileleni mwili hutoa homoni za Endorphins ambazo huhusika na kuufanya mwili ujisikie vizuri na kuchochea furaha na kujiamini. Pia hupunguza maumivu ya mwili. (1,2)
Kazi za kujipatia kipato huwa na changamoto nyingi, anza kwa kutoa wasiwasi asubuhi kabla ya kazi.
2. Zoezi
Huhesabika kama mazoezi.
Kitendo hiki huunguza nishati za kutosha hivyo kuufanya mwili uwe na afya njema kwa kuweka sawa uwiano wa nishati yake. (3)
Watu wengi hawafanyi mazoezi, pengine wewe ni mmoja wao. Sasa unajua nini cha kufanya.
3. Ujana
Hukufanya uonekane kijana.
Estogen huzalishwa wakati wa kujamiiana lakini wakati wa asubuhi huzalishwa kwa kiasi kikubwa zaidi, hufanya kazi muhimu ya kulainisha ngozi, kutunza unyevu, kuondoa mikunjo pamoja na kuongeza msukumo wa damu. (4)
Najua unatumia gharama kubwa kutunza urembo wako. Fikiria pia njia hii nyepesi.
4. Mapenzi na uhusiano
Huongeza upendo na kuboresha uhusiano.
Vichocheo vya Oxytocin vinavyozalishwa wakati huu huongeza msisimko wa mapenzi na kuukuza uhusiano.
Homoni hii hujulikana kama homoni ya mapenzi. Huzalishwa kwa wingi pia wakati wa kujifungua na ndiyo inaaminika kuhusika katika kutengeneza upendo unaodumu maisha yote kati ya mama na mtoto. (5,6)
Unataka mdumu hadi uzeeni? Ikumbuke morning glory.
5. Uzazi
Huboresha afya ya uzazi.
Wakati wa asubuhi, vichocheo vya testosterone huzalishwa kwa wingi. Pamoja na kufanya kazi zingine, husaidia katika kuboresha namba pamoja na maumbo ya mbegu za kiume ili zirutubishe yai vizuri. (7)
Wanaume, hii ni fursa kwenu.
6. Hedhi
Hupunguza maumivu ya hedhi kwa wanawake wanaopitia changamoto hii.
Mwanamke anapofika kileleni huifanya misuli ya kuta za tumbo itanuke na kusinyaa hivyo kufanya maumivu ya hedhi yapungue kwa kiasi.
Kemikali za furaha huzalishwa pia kwa wingi wakati wa asubuhi hivyo kumuandaa kikamilifu katika kupunguza maumivu ya hedhi pindi yatakapokuja. (8)
7. Tendo Zuri
Ni nzuri kwa afya.
Huchangamsha mwili, huboresha msukumo wa damu, hupunguza nafasi ya kuugua magonjwa ya moyo na saratani ya tezi dume, huongeza uwezo wa kinga mwili na hupunguza maumivu ya kichwa hasa yanayosababishwa na kipanda uso. (9,10,11)
Unasubiri nini kupata faida hizi? Changamka.
Muhtasari
Pamoja na uwepo wa faida hizi, bado muda hauwezi kuwa kikwazo cha kushiriki tendo hili muhimu.
Wapenzi wanao wajibu wa kuchagua wenyewe lini na wakati gani waungane pamoja kimwili kupitia tendo hili.
Faida hizi huwepo pia kila mara unaposhiriki tendo hili.